Wandani wa kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi wameendelea kupigia debe azma yake ya kutua wadhifa wa urais kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka wa 2022 wakisema ana tajriba ya kutosha kuongoza taifa hili.

Mwanaharakati wa kisiasa katika eneo bunge la Mumias Mashariki David Wamatsi anasema muda umewadia kwa jamii ya Magharibi kumuunga mkono Musalia Mudavadi kwani ana uwezo wa kuongoza taifa hili.

Akizungumza katika eneo la Indangalasia eneo bunge la Mumias Mashariki Wamatsi amewataka wakaazi wa Magharibi kutumia idadi kubwa ya kura zao kuamua mstakabali wa siasa za nchi hii kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Amemtaka Mudavadi kuendelea kuzuru maeneo mengine nchini kunadi sera zake na kuwatafuta marafiki wengine wa kisiasa.

Wamatsi ambaye ametangaza azma ya kumbandua mbunge Benjamin Washilai kwenye uchaguzi mkuu ujao amesisitiza kuwa atawania tena kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ANC akiwarai wakaazi kumuunga mkono.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE