Lubao FM | 102.2 Hz

Viongozi wa makanisa katika kaunti ya Kakamega wameelezea matumaini ya kufunguliwa Kwa makanisa wakati rais Kenyatta atalihutubia taifa kuhusu hali ya corona

Akiongea kwenye mazishi ya mama Dina Achimbo eneo la Elukho Butsotso Mashariki askofu Naftali Malanga wa kanisa la Church of God Ingotse mission kanda ya kati amesema kama kanisa wako tayari kuendeleza masharti ya kuthibiti msambao wa corona

Naibu chifu wa kata ndogo ya Indangalasia Scholastica Jirongo ambaye alihudhuria mazishi hayo amewahimiza wananchi kuzingatia mwongozo ambao umepeanwa na wizara ya afya

Bi Scholastica vile vile amewahimiza wazazi kuona kwamba wanapeleka watoto shuleni juma lijalo

Wazazi watoto wenu waende shule wakati shule zinafunguliwa. wasibaki nyumbani kwamaana sitaruhusu kabisa nitatembea nyumba kwa nyumba kuhakikisha watoto wote wa umri ya kwenda shuleni wanameenda shuleni.

By Lindah Adhiambo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE