Serikali ya kitaifa kupitia bodi ya hazina ya CDFC imetakiwa kuhakikisha kuwa fedha za maeneo bunge zinatumwa kwa wakati unaofaa.
Mwenyekiti wa hazina ya CDFC eneo bunge la Nambale kaunti ya Busia Vincent Okochil na msaidizi wa mbunge wa Nambale Samwel Wandera wanasema kucheleweshwa kwa fedha hizo kunaathiri pakubwa utekelezwaji wa miradi na viwango vya elimu katika eneo hilo.
Okochil ameelzea kujitolea kwa kamati ya CDFC ya Nambale katika kuboresha viwango vya elimu kupitia hazina hiyo.
Waliyasema hayo katika afisi ya CDF Nambale wakati wa hafla ya kuwakabidhi wanafunzi wa shule za upili hundi za fedha za basari za mwaka wa 2020-2021.
CDF namba
By Hillary Karungani