Chifu wa kata ya Butsotso Mashariki katika kaunti ya Kakamega Justus Mukoshi amewatahadharisha wakazi dhidi ya kutangamana kiholela katika hafla za mazishi wakati huu wa vifo vingi visivyoeleweka msimu huu wa janga la Corona
Akiwahutubia waombolezaji katika eneo la Emmachembe kwenye mazishi ya Alex Afubwa ambaye alikuwa msimamizi wa miradi ya kijamii Mukoshi amesema janga la Corona Limejificha katika hali isoyoeleweka na ni muhimu kwa wakazi kuwa macho
Mukoshi aidha amewataka viongozi wa makanisa kuzingatia maagizo yaliyowekwa na kusubiri mwelekeo wa serikali
Ni usemi uliosisitizwa na mwenyekiti wa kamati ya dini kuhusu janga la Corona katika kaunti ya Kakamega askofu Nicholas Olumasai akiwataka viongozi wa makanisa kuwa watiifu
By Lindah Adhiambo
