Shinikizo zinazidi kutolewa kwa serikali kuruhusu makanisa kuendeleza ibada kwa kuzingatia masharti

Wakiongea eneo la Sabatia Butere kwenye mazishi ya mama Truphena Sakwa mkewe mchungaji David Sakwa viongozi wa makanisa ya PEFA kupitia kwa Elly Onyango wamesema suluhu la changamoto ya Corona lipo kwenye makanisa

Tunaomba tu serikali itufungulie makanisa. Hamuwezi funga makanisa na munafungulia pahali pengine. sisi ka wachungaji tumeshidwa kuelewa corona iko tu kwa Kanisa lakini kwa vilabu hakuna? Kanisa ndio mambo yote kwa maana mtu huenda Kanisa kusali na anapo Sali hata iyo corona inamuepuka kwa hivyo serikali tunaomba utufungulie Kanisa. Hapo kwa Kanisa bado tunazingatia masharti yote


Ni usemi uliosisitizwa na mchungaji Sylvano Mumia ambaye amesema ni changamoto hasa Kwa kuwalea vijana makanisa yakiwa yamefungwa

Kwa upande mwingine wachungaji hawa kupitia kwa Shadrak Wakhu wameitaka serikali ya kaunti ya Kakamega kuimarisha hali ya matibabu kuwapunguzia wakazi mzigo

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE