Mvutano unaendelea kushuhudiwa baina ya viongozi wa kisiasa kutoka eneo bunge la Mumias Mashariki wakionekana kutofautiana kutokana mahali hospitali ya level 4 inastahili kuwekwa eneobunge hilo baadhi yao wakipendekeza hospitali ya Makunga ipandishwe kiwango cha kuwa level 4 huku wengine wakipendekeza iwekwe mjini Shianda.
Wakizungumza katika kijiji cha Ikoli , eneobunge la Mumias Mashariki kwenye mazishi ya Rodgers Makokha nduguye mwanasiasa kutoka maeneo hayo Steven Makokha wanasiasa hao wananyosheana kidole cha lawama kutokana na pendekezo la kujengwa kwa hospitali ya level 4 eneobunge hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wadi wa Malaha/Makunga/ Isongo Lucas Radioli aliyekuwa amehudhuria mazishi hayo aliwataka wanasiasa kukoma kuingiza siasa katika swala la hospitali akidokeza tayari mikakati imeanza ya kuiunda hospitali ya Makunga kuwa kiwango cha level 4 na kuongezea bado hospitali ya Shianda itapandishwa kiwango cha level 4 kutokana na chuo cha matibabu kilicho maeneo hayo
Naibu wa chifu wa kata ndogo ya Makunga James Rapando amewataka wazazi kutafuta namna ya kuwapeleka watoto shuleni kwa muhula wa kwanza kando na kuwatafutia taasisi , na vyuo mbalimbali vya ufundi kwa wanao waliokamilisha mitihanio yao ya darasa la nane na kidato cha nne mtawalia.
Ni mazishi yaliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa Lurambi Askofu Titus aliyedinda kuongelea siasa huku akiwataka wananchi kuzifwata sheria za wizara ya afya kama njia mojawapo ya kupigana na janga la covid 19.
By James Nadwa