Mbunge wa Sirisia John Koyi Waluke amewahimiza vijana kwenye kaunti ya Bungoma kujitenga na wanasiasa ambao nia yao ni kuwagonganisha na kuwatumia kuzua vurugu kwenye hafla mbalimbali hasa za mazishi.

Akizungumza kwenye mkutano uliowaleta pamoja wanachama wa U.D.A kwenye mkahawa mmoja mjini Bungoma, Waluke amesikitikia misururu ya vurugu kwenye hafla za mazishi kwenye kaunti hiyo akiwashauri vijana kuwaunga mkono wanasiasa wenye ajenda ya kuwainua kimaisha.

Wakati uo huo Waluke amewasihi wakaazi wa kaunti ya Bungoma na taifa kwa jumla kujiandikisha kwenye chama cha U.D.A. huku akiwahimiza wananchi kuuunga azma ya naibu rais dakta William Ruto ya kuingia ikulu baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Anasema hatua ya kufanya kazi kwa karibu na serikali ya kitaifa imepelekea eneo hilo kunufaika pakubwa kimaendeleo, huku akiwapongeza wakaazi wa eneobunge la Kiambaa kwa kumchagua John Njuguna Wanjiku kama mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo ulioandaliwa hapo jana.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE