Huku serikali ikiwekea vikwazo vipya vya kupunguza mkurupuko wa corona nchini kwa takribani kaunti 13 kote nchini, sasa imeshauriwa kufikiria upya katika swala hilo
Kulingana na mwanasaikologia Phillis Kibiriti katika kaunti ya Busia masharti hayo mapya hayalemazi tu ukanda huu wa magharibi kiuchumi bali ina madhara makubwa kwa saikologia haswaa ya wanainchi waliolemewa na mzigo wa kiuchumi
Kiberiti amehoji kuwa hayapingi masharti hayo mapya moja kwa moja ila anapendekeza kuwa masaa ya kuanza curfew ingesongeshwa mbele kidogo ili kumpa mwanainchi wa kawaida nafasi ya kurejea nyumbani bila kuhangaishwa huku akisema kuwa masaa yaliyowekwa ya saa moja jioni ni mapema mno
Kuhusiana na swala la kuyafunga maeneo ya kuabudu,Kibiriti ametilia shaka uamuzi huo huku akimrai rais Uhuru Kenyatta kukaa chini na viongozi wa kidini na kuutathmini upya msimamo huo
Ikumbukwe kuwa viongozi wa kidini wameukashfu uamuzi wa Rais Kenyatta kuyafunga maeneo ya kuabudu huku wakiutaja kama usio faa.