HUKU timu ya taifa Harambee Stars ikitarajiwa kumenyana na Misri katika mechi ya kufuzu Taifa Bingwa Afrika (AFCON) Alhamisi, mashabiki wanasubiri kuona nani mkali kati ya mshambuliaji matata Michael Olunga na nyota wa Liverpool, Mohammed Salah.
Kikosi cha Misri kinachoshirikisha Salah na Mohamed Elneny wa Arsenal, kimewasili nchini tayari kwa ngarambe hiyo itakayosakatwa uwanjani Kasarani kuanzia saa moja jioni.
Salah amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu na ingawa fomu ya Liverpool imekuwa mbovu katika mechi za hivi karibuni, ndiye anaongoza chati ya ufungaji katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa mabao 17.
By Samson Nyongesa