Huku shughuli za mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE zikikamilika hii leo kote nchini
Serikali kupitia wizara ya elimu na tume ya kusimamia mitihani nchini KNEC imepongezwa kwa juhudi njema ilizoweka wakati wa mitihani hiyo iliyong’oa nanga jumatatu wiki hili na kukamilika vyema
Ni kauli yake mkurugenzi mkuu wa shule ya msingi ya Hilltop Sherry Academy iliyoko kwenye barabara kuu ya Lubao-Cheviso Geoffrey Agesa
Akizungumza moja kwa moja na kituo hiki Agesa ameelezea matumaini yake ya watahiniwa wa shule hiyo kuandikisha matokeo bora kwenye mtihani akipongeza juhudi za walimu,wazazi na wanagunzi wa shule hiyo kwa kutia bidii
Nao watahiniwa wa shule hiyo pia wakipongeza wizara ya elimu na idara ya mitihani nchini KNEC kwa maandalizi mema wakitarajia kufanya vyema kwenye mtihani huo
By Javan Sajida