Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na nyuki wakiwa bomani mwao katika kijiji cha Lukhokho kata ya Lwandeti eneobunge la Lugari kaunti ya Kakamega.
Inadaiwa nyuki hao walikuwa wamekita kambi kwenye mti mmoja shambani mwa jirani yao kabla ya kuchokozwa na mwewe aliyewafanya wawavamie watoto hao huku mamake mwendazake bi. Phanice Nelima akielezea kusikitishwa na kifo cha mwanawe
Kwa upande wake nyanyake mwendazake bi Jemima Milenja amesema alikuwa akimshugulikia mumewe hosipitalini wakati alipopashwa habari hizo za huzuni.
Kulingana na manusura nyuki hao hawakuwauma majirani waliojitokeza kuwasaidia ila waliilenga tu jamii hiyo huku familia hiyo ikihoji nyuki hao sio wa kawaida..
By Samson Nyongesa