Mzozo wa ardhi unazidi kutokota Kati ya familia moja mtaa wa Makunga na chifu wa lokesheni ya Isongo wilayani Mumias Mashariki Harrison Keya Oluye

Kulingana na Mzee Sakwa Omusikoyo chifu huyo ameingilia mzozo wa ardhi haswa kufunguliwa kwa njia Kati yake na ndugu yake 

Hii imefanya wao kushindwa hata pa kumpitishia marehemu mojawapo wa  nduguze amabaye aliaga dunia wiki moja ilopota

Hiyo njia tulizaliwa Kama iko na imefungwa na watoto ambao tumezaa. sasa serikali itusaidie iende kwa map kwa sababu wananchi wamefungua kwa nguvu na sasa inaleta ugomvi kwa familia

Mkaazi huyo amemsuta chifu kwa kile alichokitaja kama kushirikiana na nduguye kumnyanyasa na kufanya mzozo huo kutokota hata zaidi

Sakwa amemnyoshea chifu huyo kidole Cha lawama kwa kuvuruga familia yake hata kwa kumsingizia makosa ya wizi wa ng’ombe akitishia kumchukulia hatua

Juhudi zetu za kuzungumza na chifu huyo hazikufua dafu baada yake kudinda kupokea simu zetu ikidaiwa kuwa yuko katika shuguli muhimu ya kiserikali

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE