Idadi ya juu ya watoto wanaofika hospitalini wilayani Khwisero wameathirika na magonjwa ambukizi haswa aina tofauti za homa

Afisa msimamizi wa kituo cha afya Cha SONAC wilayani Khwisero Solomon Akali Omuroka ametaja ugojwa wa Chickenpox kama sugu haswa kwa watoto chini ya umri wa miaka 10

Saizi watoto wengi wameadhirika na huu ugojwa wa chickenpox. na ukianza mtoto anakua na dalili za homa na maleria, na unaambukizana. Ningewasii wazazi wakati mtoto anaonesha hizo dalili mfikishe hospitalini kwa haraka.

Afisa huyo ametaja dalili za awali sawa na za malaria  na kuwataka wazazi kumakinika na dalili hizo kwa watoto wao

Mtaalamu huyo wa matibabu amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao Mara kwa Mara kwenye vituo vya afya kukaguliwa ili kuwezesha tiba ya mapema

Ningewasii wazazi kwamba wapeleke watoto mara kwa mara katika vituo vya afya kuangaliwa hata kama hawana dalili zozote ili kuzuia maabukizi na matibabu ya mapema.

Utafiti unaonyesha kuwa mtoto 1 kati ya 4 huugua ugonjwa huu wilayani humo kila wiki

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE