Kanisa Katoliki nchini limewataka maafisa wa usalama kutumia kamati za makanisa zilichaguliwa kushughulikia masharti ya korona makanisani.
Akiongea wakati wa Upadrisho kwa mapadri sita katika uwanja wa seminari ndogo ya Petro Mukumu eneo bunge la Shinyalu, askofu wa kanisa hilo Jimbo Katoloki la Kakamega Rt Rev Joseph Obanyi, amesema mara nyingi vitengo vya usalama vimekuwa vikiangaisha waumini kanisani akitaka kuwepo kwa utaratibu.
“Si vizuri wakristu kuangaishwa wakati wako kanisani wakati wa ibaada. Maafisa wa usalama wafaa kushirikiana na kamati za makanisa za kushughulikia masharti ya korona ili waweze kuelewa jinsi Kanisa linavyo pambana na vita dhidi ya ugojwa wa korona. “ alisoma Askofu Obanyi
Aidha amewataka mapadri kuzingatia sheria zilizowekwa za korona wakati wanapo adhimisha misa takatifu na pia wakati wanapo fanya sherehe zozote zile kanisani kama ubatizo.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na kiranja wa bunge la kitaifa Emmanuel Wangwe, mbunge wa Mumias Mashariki Benjamin Washiali, mbunge wa Shinyalu Justus Mugali na mbunge wakaunti ya bi. Elsie Muhanda.
By Imelda Lihavi