Mbunge wa Lurambi askofu Titus Khamala amemtaka mwenzake wa Kimilili Didmus Barasa kufanya uamuzi wa kushirikiana na kinara wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangula kufuatia hatua yake ya kujipatia likizo ya miezi minne kufanya uamuzi wa mwelekeo wa kisiasa

Akiongea alipokabidhi hundi ya kununua shamba la shule ya msingi ya Elufwafwa wadi ya Butsotso Mashariki hapo jana Khamala amesema Barasa ana haki ya kujipatia likizo lakini matarajio ya jamii ya waluhya ni kwamba atafanya uamuzi wa kuungana na viongozi wengine wa waluhya kukuza nguvu zao za kisiasa

 Khamala vile vile amewasuta baadhi ya wapinzani wake kwa kuwatumia vibaya vijana kuharibu sifa za viongozi kwenye mitandao ya kijamii na kuwataka vijana kuepuka na kutumiwa vibaya kisiasa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE