Wito umetolewa kwa viongozi wa siasa kutoka eneo bunge la Mlima Elgon kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushirikiana kikamilifu katika kutekelezea wakazi maendeleo kwa muda uliosalia kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu ujao

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa  jamii ya Sabaot, Stephen Musani ambaye anahoji kuwa inasikitisha kuona wawakilishi wadi kutoka eneo hilo hawana uhusiano mwema na mbunge Fred kapondi akiwataka kushirikiana kwa manufaa ya mwananchi wa kawaida.

Aidha Musani ameongeza kuwa eneo bunge la Mlima Elgon ni sharti ligawanywe ili kupata maeneobunge mawili akisema hatua hiyo itasitisha hulka ya baadhi ya wakaazi wanaoishi karibu na mipaka kujisajili katika maeneobubge mengine msimu wa uchaguzi.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE