waziri wa afyya Kenya, Mutahi Kagwe

by Imelda Lihavi

Idadi ya maambukizi ya virusi vya korona nchini imezidi kuongezeka sawia na visa vya wanao pona kutokana na ugonjwa huo. Kufikia hii leo idadi ya maambukizi imefikia 3,727 baada ya visa vingine 133 vya maambukizi kuripotiwa kwa sampuli 3,365 katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Akihutubia taifa katika kaunti ya Nyandarua hii leo, waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe ameeleza kuwa watu wengine 33 wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya kupata nafuu na kufikisha watu idadi hio 1,286.Aidha Mutahi, ametangaza kufariki dunia kwa mtu mmoja na hivyo kufikisha 104, idadi ya waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19

 Kaunti ya Nyandarua ni miongoni mwa kaunti 9 nchini ambazo hazijasajili kisa chochote cha corona na hivyo waziri wa afya Mutahi amewahimiza viongozi na washikadau wa kaunti hio kushirikiana kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeingia katika kaunti hiyo kiholela.Vilevile kagwe amewataka wakenya kuzingatia na kufuata masharti ya serikali kama njia ya kupunguza maambukizi. Gavana wa nyandarua Francis Kimemia ameeleza kuwa jimbo hilo limetenga vitanda vya wagonjwa mahututi (ICU) 13 na ambavyo vilinunuliwa kwa shilingi milioni 70. Pia alieleza kuwa wametenga vitanda vingine 300 vya kuwatenga wagonjwa.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE