Mbunge wa Ikolomani Benard Shinali ameelezea kusikitishwa kwake na idadi kubwa ya watu wanaotoka kaunti zingine kuja eneo lake kutafuta dhahabu bila ya ufahamu wa idara ya utawala.

Akihutubia waombolezaji kwenye mazishi kijiji cha Mubunge mpakani mwa eneo bunge lake na Lurambi, Shinali amewataka wale wanaokuja eneo hilo kujitafutia riziki kuhakikisha wanajifahamisha kwenye idara za utawala na zile za kaunti na hata afisi yake ili kubaini wageni walioko sehemu hiyo.

Shinali anasema hii inajiri siku chache baada ya watu watano kupoteza uhai wao walipofunikwa na mchanga huku wanane wakiokolewa , kupelekea tatanishi ya idadi kamili ya waathiriwa kwa kukosa majina ya watu wanaojihusisha na uchimbaji wa dhahabu eneo hilo.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE