Huku wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa KCPE mwaka jana wakitarajiwa kujiunga na shule za upili wazazi kutoka eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega wametakiwa kutofuja kiholela fedha zao na badala yake kuekeza vyema kwa ajili ya karo ya wanao

Ni kauli yake chifu wa kata ya Silungai Nixon Teka ambaye amewataka wazazi kutofuja fedha zao ovyo  na vile vile kuwa waangalifu na wanao muda huu wamaposalia nyumbni wakisubiri kujiunga na shule za upili.

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha hamtua eneo bunge la Malava mtawala huyo kadhalika ametoa onyo kwa wale wanafunzi ambao hurandaranda ovyo barabarani  badala ya kufika shuleni akihoji kuwa wataadhibiwa kulingana na sheria.

Aidha teka ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kuendelea kuzingatia masharti ya wizara ya afya katika juhudi za kupigana na janga hatari la covid 19.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE