Manchester United wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo huku klabu hiyo ya Italia ikiwa iko tayari kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 36 kwa kubadilishana na kiungo wa kati Paul Pogba mwenye umri wa miaka 28
Hayo yakijiri Tottenham wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus mwenye umri wa miaka 24 ambapo itashuhudia kubadilishana na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane pamoja na nyongeza ya fedha
Na kule Real Madrid Kiungo wa kati Dani Ceballos, amesema anataka kusalia Real Madrid msimu ujao au kuondoka kabisa kwenye klabu baada ya kutumia misimu miwili akichezea klabu ya Arsenal
By Samson Nyongesa