Huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kuzuru mko wa magharibi mwa nchi hivi karibuni viongozi kutoka jamii ya mulembe wametakiwa kukoma kupiga siasa zisizokuwa za manufaa na badala yake kujadili mbinu mwafaka ambazo eneo hilo litanufaika kutokana na ziara hiyo.

Ni wito ambao umetolewa na Balozi Ligavo Ambeyi ambaye anahoji kuwa ziara yake rais eneo hili ni ya umuhimu zaidi na ambayo inapaswa kuleta maendeleo katika eneo hili la mkoa wa  magharibi mwa nchi.

Ambeyi vile vile anasema kuwa iwapo rais ataandamana na kinara wa ODM Raila Odinga basi inapaswa kuwa ni kwa misingi ya maendeleo na wala si kisiasa.

Balozi huyo aidha amesikitishwa na swala la kuongezwa kwa karo katika baadhi ya vyuo vikuu nchini huku akimsihi rais Kenyatta kuingilia kati na kuleta suluhu mwafaka kuhusiana na swala hilo

Ambeyi ambaye pia anakimezea mate kiti cha ubunge cha Shinyalu ametumia fursa hiyo kumpigia debe kinara wa ANC Musalia Mudavadi kutwaa uongozi wa taifa hili kwenye uchaguzi mkuu ujao.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE