Tumekua tukiwasoma kwa vitabu vya historia kama jamii ambayo ina mizizi yake nchini afrika kusini, jamii ya Shona ni kabila linalozungumza kibantu chimbuko lake ikiwa ni nchi ya Zimbabwe.  Inaaminika kua jamii ya shona haina utaifa ata baada ya kukaa Kenya zaidi ya miaka 50 jambo lililomfanya waziri wa mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa, Fred Matiangi aliipa jamii cheti cha uraia.

Matiangi aliagiza taasisi zote za elimu nchini kuruhusu udahili kwa watoto kutoka jamii ya washona ambao walikuwa na shida kupata elimu kwa sababu ya kutokuwa na utaifa. Watu wa shona walifika Kenya mnamo 1959 wakiwa wamishonari wakati Kenya ilipata uhuru kutoka kwa waingereza mnamo 1963. Hawakuweza kudhibitisha uhusiano wao wa kisheria kwa nchi zao za asili kama inavyotakiwa na sheria inayosimamia usajili wa vizazi na uraia nchini kenya.

Kenya pia ilitangaza itatoa uraia kwa jamii ya Sagaf ya Tana River, ambayo itakuwa kundi la mwisho la watu wasio na utaifa wakipata vitambulisho.

Mnamo mwaka wa 2016, watu 1,496 wa jamii ya Makonde wanaoishi katika kaunti ya kwale walisajiliwa kirasmikama wakenya baada ya serikali kuwapa uraia.

By Wycliffe Andabwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE