Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa mikusanyiko yote ya umma imeahirishwa kufuatia kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya COVID-19 humu nchini.

Waziri Kagwe alisema kuwa muda wa kafyu kote nchini umeongezwa kwanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri kote nchini.

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa katika jumba la Harambee, Waziri huyo alidokeza kuwa mikutano kadhaa ya serikali pia imeahirishwa.

Aidha Kagwe alisema visa vya maambukizi vimeongezeka katika kaunti za Kiambu, Kajiado, Lamu, Makueni Muranga, Taita Taveta na kwa mara ya kwanza katika kaunti ya Tana River.

Waziri wa afya vilevile aliwahimiza waajiri kuwaruhusu wafanyikazi kufanyia kazi nyumbani kulingana na haja ilivyo.

Aliagiza kwamba sehemu za ibada ziwe na watu thuluthi moja kulingana na idadi ya kawaida ya wakristo kwa kuzingatia kikamilifu sheria za kuzuia msambao wa homa ya corona huku waumini wakitakiwa kuwa umbali wa angalau mita moja.

Hoteli na sehemu za burudani zimetakiwa kuendeleza shughuli zao kulingana na sheria zilizo wekwa na wizara ya Afya.

Vile vile  Kenya inatarajiwa kupokea dozi 400,000  za chanjo ya AstraZeneca kutoka kwa serikali ya Uingereza.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE