Muungano wa makanisa NCCK kanda ya Magharibi unaitaka serikali kutafuta mbinu bora za kukabili maambukizo ya corona pasipo kuyakwamisha maisha ya wakenya
Wakiwahutubia wanahabari baada ya mkutano wao mjini Kakamega kupitia kwa naibu mwenyekiti askofu Sinema Bamba wamesema kufunga nchi bila kuwapa wananchi suluhisho la hali ngumu ya maisha hakutazuia msambao huo
Viongozi hawa wa kidini vile vile wanazitaka idara husika za serikali kuthibiti makali ya kisiasa na kuwachukulia hatua wale wanaochochea uhasama ambao unaweza kuitumbukiza nchi hii kwa machafuko
By Imelda Lihavi