Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane mwenye umri wa miaka 27, atakuwa mlengwa wa Manchester City ikiwa viongozi wa Ligi ya Primia watashindwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland msimu huu.
Vile vile Manchester City na Chelsea zote zimembaini mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku, 27, raia wa Ubelgiji kama mchezaji wao mbadala ikiwa zitashindwa kumsajili Haaland mwenye umri wa miaka 20
Hata hivyo, City ina imani kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway Haaland msimu huu kama mbadala wa Sergio Aguero.
By Samson Nyongesa