Huku ikisalia takriban mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa nchini, viongozi wa kisiasa wameanzisha mchakato wa kuwaleta pamoja viongozi wa kisiasa na wale wa kidini kwa lengo kuhakikisha kuwa amani inazingatiwa pakubwa kabla na hata baada ya  uchaguzi huo mkuu wa mwaka 2022.

 Ni juhudi la kanisa la Marafiki eneo la Africa likiongozwa na Bainito Wamalwa anayedai kuwa ni jukumu la kanisa kuhakikisha kuwa usalama na amani unazingatiwa na hili litawezekana tu iwapo viongozi wa kisiasa watashirikishwa.

Naibu Gavana wa kaunti ya Vihiga dakta Patrick Saisi akilizungumzia hili,amelitaka kanisa kuwakubali na kuwaelekeza wanasiasa bila ya kuwabagua.

Aidha dakta Saisi amelitaka kanisa kuzingatia kutoa mwelekeo kwa wanafunzi kukabili changamoto ya ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Kando na haya pia ameomba uelekezi kuhusiana na mswada wa marekebisho ya katibaa ya BBI kwa wakazi.

Story by Alovi Joseph

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE