Vijana kutoka Elgeyo Marakwet wametoa hisia tofauti dhidi ya mchakato wa BBİ kupitishwa au la katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Kulingana na kiongozi wa vijana kutoka eneo la Elgeyo Marakwet İsaac Cherono Rotich akihutubia wanahabari amesema kuwa msuada wa BBİ kupitisha ama la italingana na gavana wa kaunti Ya Elgeyo Marakwet  Alex Tolgos kuangalia kama itawafaidi wananchi.

“kwa sasa gavana ndio kiongozi mkuu wa eneo hilo na tunajua kuwa amesoma na akaelewa na kama ni mzuri county government itapitisha na kama ni mbaya haitapitishwa.”

Bali na hayo İsaac cherono ameongeza kuwa siasa kati ya “Dynasty na hustler” itatenganisha wananchi kulingana na uwezo bali si kuwaleta pamoja.

“Hizi movement za Dynasity na Hustler itatuletea utengano nnchini kwa maana inaelezea uwezo wa binadamu maskini ama tajiri hii ni kutenganisha jamii ya wakenya sasa sisi kama vijana yafaa tuchungane nazo”

Aidha, Dennis kipkoech akiwa miongoni mwa vijana kutoka Elgeyo Marakwet amesisitiza kuwa serikali inapaswa kuwawezesha vijana ilhali haifai kuwatumia vibaya hasa kwa kuwapa hongo ili waendeleze vita wakati wa siasa.

Story by Sharon Lukorito

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE