Katibu mkuu wa elimu Alfred Cheruiyot leo hii ametembelea kaunti ya Uasin Gishu na ataweza kukagua shule mbali mbali ili kuweza kuangalia changamoto ambayo imekuwa ikiwakumba hasa wanapoendeleza masomo wakizingatia masharti ambayo yaliwekwa na waziri wa wizara ya Elimu George Magoha.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu huyo amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa shule zimeweza kukabiliana na masharti yaliowekwa hata hivyo shule hizo zitaweza kutaja changamoto ambayo imekuwa ikiwakumba wanapoendeleza masomo yao.

Hata hivyo waziri wa elimu kutoka kaunti ya Uasin Gishu Joseph Kurgat amesihi kuwa wameshirikiana na machifu kwa kuhakikisha wanafunzi wote wamerejelea shuleni hii ikiwa agizo ambayo rais Uhuru Kenyatta alipeana baada ya kuruhusu shule kufunguliwa. 

story by Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE