Bunge la kaunti ya Kakamega linapania kufanyia marekebisho  mswada wa Imarisha Afya ya Mama na Mtoto uliopitishwa mwaka 2017 na kuanzisha mpango wa kuwasaidia akina mama hao ukiwa pamoja na wahudumu wa kujitolea wa afya .

Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni kutoka kwa wananchi juu ya kauli hiyo ya marekebisho, mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge hilo ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Isongo Makunga Malaha Lukas Radoli amesema kuwa mswada huo ulijumuisha vipengee tofauti zikiwemo za wahudumu wa afya wa kujitolea nyanjani ambao anahoji watatengezewa mswada wao ambao utashukulikia kwa karibu masilahi ya wahudumu hao.

Swala hili la masilahi ya wahudumu wa afya Nyanjani Community Health Volunteers (CHVS) litaleta afueni iwapo kutabuniwa mswada wa kuwawezesha kufanya kazi kwa mazingira bora na kulipwa marupurupu yao kwa wakati jinsi anavyosema mmoja wa wahudumu hao Patrick Lumumba.

Lumumba amesema kuwa tangu serikali za ugatuzi kuanza wahudumu hao wamekuwa wanapitia hali ngumu nyanjani ikiwemo kucheleweshwa kwa marupurupu yao.

Mambo mengine ambayo yatarekebishwa kwenye mswada huo ni kiwango cha elimu ya wasimamizi ambapo imetolewa kutoka shahada ya digree hadi ya diploma na kumpa pia majukumu msimamizi wa kifedha katika mradi huo .

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE