Serikali ya kaunti ya Kakamega imewaajiri kazi wauguzi wapya 61 kwa kandarasi ya muda wa miaka mitatu ili kuziba pengo ambalo limeachwa na wauguzi ambao wanashiriki kwenye mgomo.

Akihutubia wauguzi walioajiriwa mjini kakamega, Gavana Wycliffe Oparanya amewaonya wauguzi dhidi ya kuasi majukumu yao ambayo waliapa kutekeleza.

Oparanya pia amedokeza kwamba amemuagiza waziri wake wa huduma ya umma kuwaajiri wauguzi wengine 90 zaidi, ambao wanafaa kuripoti kazini tarehe 1 mwezi Machi mwaka huu.

Aidha gavana huyo amedokeza kwamba wauguzi ambao wanashiriki mgomo hawatalipwa mishahara yao kwa kuwa wanakiuka agizo la mahakama la kurejea kazini.

Wahudumu wa afya walianza mgomo mnamo tarehe 7 mwezi Disemba mwaka uliopita hadi kufikia wakati huu, jambo ambalo limeathiri pakubwa huduma za afya katika hospitali za umma.

Story By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE