Kiwanja cha Kipchoge mjini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu kitakamilika kabla ya mwezi wa tano mwaka huu.

Waziri wa michezo Amina Mohammed alinena maneno haya baada ya kukagua kiwanja cha Kipchoge Keino na kusema kuwa wanariadha wanatakina kutumia kiwanja hicho kuendeleza mazoezi kabla ya kuenda mashindano Tokyo mwezi wa Agosti.

Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amesihi kuwa kiwanja hicho kikikamilika kitaleta faida kwani huenda siku moja kitatumika kwa mashindano ya dunia mzima.

Aidha, mkarandarasi aliyekuwa akisimamia kiwanja cha Kamariny kutoka eneo la Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet kandarasi yake imetupiliwa mbali baada ya kukosa kukamilisha ujenzi kwa muda aliyopewa na waziri wa michezo Amina Mohammed.

Hayo yakijiri baada ya ujenzi wa kiwanja cha Kamariny kilianzishwa mwezi wa Juni mwaka wa 2020 ambapo mkandarasi huyo alifaa kukamilisha mwezi wa Agosti.

Story By Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE