Hatua ya gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya kuwatimua kazi wahudumu wa afya wanaogoma na kuanza kuwaajiri wauguzi wapya, imekashifiwa na viongozi wa kidini kutoka kaunti hiyo wanaopendekeza mazungumzo ya kina ili kulitatua tatizo hilo.
Wakizungumza muda mchache tu baada ya gavana Oparanya kufanya uamuzi huo, muuungano wa kidini kaunti ya Kakamega chini ya mwenyekiti wake Askofu Nicholas Olumasai wameukosoa msimamo mkali wa Oparanya wakisema utaleta uhasama miongoni mwa wakazi.
wanapendekeza mazungumzo kati ya Rais Uhuru Kenyatta, Gavana Oparanya na katibu wa chama cha wauguzi nchini Seth Panyako ili kutatua mvutano uliopo miongoni mwao.
Huku haya yakijiri wakati katibu wa chama hicho cha wauguzi katika kaunti ya Kakamega Renson Bulunya akimsuta gavana Oparanya kwa kutotilia maanani matakwa ya wauguzi na kushikilia msimamo kuwa mgomo huo ungaliipo.
Serikali ya kaunti ya Kakamega imewaajiri wauguzi wapya 61 kwa kandarasi ya muda wa miaka mitatu ili kuziba pengo ambalo limeachwa na wauguzi ambao wanashiriki kwenye mgomo huku akimwagiza waziri wake wa huduma ya umma kuwaajiri wauguzi wengine 90 zaidi, ambao wanafaa kuripoti kazini tarehe 1 mwezi Machi mwaka huu.
Story by Boaz Shitemi