Klabu ya Tottenham imewasiliana na kiungo wa kati wa PSG na Argentina Angel di Maria kuhusu uhamisho wa kwenda London. Mchezaji huyo wa zamani wa Man United mwenye umri wa miaka 32 anapatikana kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu. 

Hayo yakijiri PSG bado inatumai kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia . Spurs inafikiria kumsaini kiungo mchezeshaji wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus, 23, kama mtu atakeyechukua nafasi yake. 

Spurs pia imehusishwa na uhamisho wa beki wa Napoli na Serbia Nikola Maksimovic, 29, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu. 

Kwingineko ni kwamba Thomas Tuchel amedaiwa kutopoteza muda katika mipango ya siku za usoni ya Chelsea kama mkufunzi wa klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani ambaye alichukua mahala pake Frank Lampard katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumanne amesema beki wa klabu ya RB Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, ni miongoni mwa wachezaji anaowalenga sana. 

Kufutwa kwa Lampard kumeiwacha klabu ya West Ham ikiwa na matumaini kwamba hamu ya Chelsea ya kumsajili mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 22 itakuwa imeisha. 

Na Beki wa kushoto wa Chelsea Baba Rahman anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kuondoka katika klabu hiyo tangu mkufunzi Lampard kupigwa kalamu , huku mchezaji huyo wa Ghana mwenye umri wa miaka 26, akitarajiwa kujiunga na klabu ya Ugiriki PAOK Salonika kwa mkopo. 

Kule Old Trafford Winga wa Manchester United Facundo Pellistri anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Old Trafford kwa mkopo huku Club Bruges na Alaves zikimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 raia wa Uruguay, ambaye alijiunga na The Red devils kutoka Penarol mwezi Oktoba. 

Tukivuka mipaka Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 30, anatarajiwa kusalia katika klabu ya Crystal Palace licha ya klabu ya West Bromwich Albion kumnyatia. 

Arsenal ina kibarua kigumu cha kushindana na Barcelona katika kumsajili beki wa kati wa Manchester City mwenye umri wa miaka 21 Eric Garcia, ambaye anatarajiwa kuondoka kama mchezaji huru mwisho wa msimu huu. 

 Story by Samson Nyongesa………*

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE