Kinara wa chama cha ANC Wycliffe Musalia Mudavadi amewakosoa walimu wakuu nchini na uhusiano wa karibu na shule hiyo
Mudavadi kwa kuwalazimisha wazazi kununua bidhaa tofauti za shule katika maduka kadhaa yaliyo amesema ni vyema wazazi kuruhusiwa kununua bidhaa za shule katika maduka wapendayo kulingana na bei na uwezo wao badala ya kuwalazimu
Wakati uo huo Mudavadi amekosoa jinsi uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza ilivyofanywa huku wanafunzi wengi wakitumwa shule zilizo mbali na kwao huku akiwasihi wakenya kumuunga mkono kwenye kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao ili kubadilisha maswala kadha yakiwemo ya elimu
Mudavadi amepongeza mtaala mpya wa elimu wa CBC japo akaitaka wizara ya elimu nchini na walimu kuwa tayari kwa uzito utaotokea mwaka ujao haswa katika swala la serikali kuweka asilimia 100 ya wanafunzi waliokalia mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE kujiunga na shule za upili nchini huku swala la miundo msingi ya shule likiwa changamoto kuu
By Javan Sajida