Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya upili ya Mundaha eneo bunge la Khwisero kaunti ya Kakamega amelazwa katika hospitali ya misheni ya Mwihila na majeraha kichwani baada ya kupigwa na nyundo na babake mzazi kwa madai ya kuuliza karo ya shule.

Beverlyne Khatondi wa miaka 18 anadai kuwa nduguye anayefanya kazi jijini Nairobi alikuwa amemhaidi kutuma shilingi elfu kumi ambazo ilifaa kulipia kiasi cha karo yake ya shilingi elfu tano na nduguye aliye katika kidato cha kwanza shilingi elfu tano mtawalia, na alipojaribu kumuuliza babake iwapo nduguye alikuwa ametuma hela hizo, alimgeukia kwa mateke na nyundo kichwani kupelekea majeraha hao mwilini na kichwani.

Mtetezi wa haki za wasichana eneo bunge hilo bi. Nancy Njomo, anasema mshukiwa  akidai kuwa mwathiriwa alitishia kumpiga ndiposa akamuadhibu kabla ya kukimbilia mafichoni baada ya kutekeleza uovu huo, akifichua kuwa sio mara ya kwanza kwa mwathiriwa kudhulumiwa na babake huku mamake mzazi akiegemea upande wa mumewe.

Muuguzi mkuu wa hospitali hiyo bi.Saum Mwaka amesema mwathiriwa alifikishwa hospitalini humo akivuja damu nyingi kutoka kichwani japo kwa sasa yuko katika hali salama.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE