Wakaazi wa lokesheni ndogo ya Buyangu wamehimizwa kuzingatia sheria za kudhibiti msambao wa virusi vya corona
Ni kauli yake naibu chifu wa lokesheni hiyo Catherine Nelima akihutubia waombolezaji kwenye ibaada ya maombi na mazishi ya mzee Renson Oyangi Magana katika kijiji cha Lusero
Nelima amewahimiza wazazi kuwapeleka wanao waliokalia mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE mwaka uliopita ikizingatiwa agizo la serikali la kuhitimu asilimia 100
Naye mwakilishi wadi wa Isukha Kazkazini eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega Hellemina Llanziva akiwahutubia waombolezaji amewatahadharisha wakaazi wake dhidi ya tapeli wanaokusanya kadi za kitaifa na kuwasajili wakenya katika mirengo mbalimbali ya kisiasa kwa kutojua huku uchaguzi mkuu ukikaribia
Llanziva amewataka viongozi na wanainchi kutimiza amani taifa linapokaribia kwenye uchaguzi mkuu akiwataka wakaazi kuwa makini na waangalifu wakati wa uchaguzi mkuu
By Sajida Javan