Wajumbe wa chama cha ODM kaunti ya Kakamega wamekuwa na wakati mgumu baada ya kufurushwa na maafisa wa polisi katika mikahawa miwili tofauti  mjini  humo, katika njama yao ya kutaka kubadili  uongozi wa chama hicho hii ni baada ya baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho kutaka  kumuidhinisha mbunge wa Shinyalu Justus Kizito Mugali kuwa mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kakamega wadhfa ambao ulikuwa ukishikiliwa na naibu gavana wa kaunti ya Kakamega Profesa Philip Museve Kutima.

Wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Kakamega viongozi hao wamekana madai ya kupindua uongozi wa naibu gavana Profesa Philip Kutima wakishikilia kwamba walifuata taratibu zote kwa kuendesha uteuzi huo na wakafiki kumpa mbunge Kitizo wadhfa huo ambao anasema ni mwamko mpya kwenye chama hicho.

Hata hivyo viongozi hao wameisuta idara ya usalama mjini Kakamega kwa kuwahangaisha kwenye mkutano wao, wakiwataka polisi kutotumiwa visivyo na wanasiasa na wale wapinzani wao kwenye chama hicho.

Licha ya hayo, baadhi ya wanachama ambao walikuwa  wameudhuria mkutano huo walionekana kutoridhishwa na mapendekezo ya baadhi ya nyadhfa za uongozi huo mpya na kusababisha vurugu ambayo mbunge Kizito aliingilia kati na kutiliza hali.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE