Wanaharakati Kaunti ya Bungoma chini ya vuguvugu la Bungoma Liberation wamekosoa hatua ya serikali ya Kaunti hiyo kuchelewesha malipo ya wafanyakazi wake ikiwemo wahudumu wa afya, hali ambayo imelemaza huduma za afya katika hospitali za umma kwa siku ya nne sasa Kufuatia mgomo wa wahudumu wa afya uliong’oa nanga Alhamisi iliyopita.

Suleiman Hamisi ambaye ni mwanachama katika vuguvugu hilo, amesema mgomo wa wahudumu wa afya umeathiri familia nyingi zinazotegemea huduma za afya katika hospitali za umma.

Kwa sasa wanaharakati hao wanamtaka Gavana Kaunti hiyo Wycliffe Wangamati kuharakakisha malipo ya wahudumu hao wa afya pamoja na wafanyakazi wengine kwenye serikali hiyo ambao hawajalipwa kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwilli.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE