Katibu wa chama cha Walimu KNUT tawi la Bungoma Kusini Kenneth Nganga amewaomba wakazi kuhakikisha kuwa wanao wanaripoti shuleni shule zinapotarajiwa kufunguliwa kwa muhula wa Kwanza baadaye mwezi huu.

Kwenye taarifa kwa wanahabari Nganga amesisitiza hasa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kusajiliwa bila kuchelewa akiwataka wazazi kutafuta karo ikiwemo Kupitia ufadhili.

Aidha amesikitikia ongezeko katika idadi ya watoto wenye umri mdogo wanaohusishwa katika biashara mjini Bungoma kinyume na sheria akiwataka wazazi kuwajibika ipasavyo.

Kufuatia hali hii sasa amewaomba Machifu na manaibu wao pamoja na wasimamizi wa mitaa kuchukua takwimu za watoto wanaohusishwa katika ajira kwa watoto badala ya kuwa shuleni ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wazazi wao.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE