Wanakandarasi katika Kaunti ya Bungoma wameanzisha mchakato wa kuwapiga jeki wale wanaolenga kusajili kampuni za kufanya kandarasi ikiwemo kutoa ushauri utakaofanikisha kampuni zao kusajiliwa.

Kwenye kikao na wanahabari, Katibu wa muungano wa wanakandarasi Kaunti hiyo Joseph Nyongesa, amesema wameanza mpango huo ili kuwaleta pamoja wanakandarasi wote kwenye Kaunti hiyo.

Nyongesa aidha amesema kwa kauli moja wanakandarasi wote wameafikia kuzindua hazina itakayowasaidia wanakandarasi kuchukua mikopo na kurejesha baadaye bila kutozwa riba.

Kwa upande wake Mwelekezi wa muungano huo  Gilbert Kapchanga amesema kama njia mojawapo ya kutathmini utendakazi wa wanakandarasi, wanalenga kuandaa mikutano ya kila mwezi ili kutatua baadhi ya changamoto wanazoopita wanakandarasi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE