Kamishna Kaunti ya Bungoma Samuel Kimiti ametoa ilani kwa wahudumu wa Bodaboda dhidi ya kuandaa maandamano kila mara wanapokuwa na tatizo, akisema maandamano si njia ya kutafuta suluhisho.
Akitoa taarifa kwa wanahabari siku moja baada ya wahudumu wa Bodaboda katika eneo bunge la Kabuchai kutishia kuandamana kwa msingi wa ukosefu wa usalama, Kimiti amesema ipo haja wahudumu wa Bodaboda sawa na wakazi wote kufuata sheria katika kuwasilisha malamishi yao.
Wakati uo huo Kimiti ametoa ilani kwa wakazi wa kaunti hiyo wanaokiuka masharti ya wizara ya afya ya kukabili virusi vya Korona ikiwemo amri ya kutopatikana nje baada ya Saa Mopjua usiku hadi saa Kumi alfajiri, akisema Polisi wanaoshika doria watawatia mbaroni wanaokiuka masharti hayo.
Ikumbukwe kuwa polisi mjini Bungoma wamewatia mbaroni watu wasiopungua Ishirini katika kipindi cha wiki moja iliyopita kwa kukaidi amri ya kutopatikana nje baada ya Saa Mojua usiku.
By Hillary Karungani