Wakaazi Wa kjiji cha Munzweyo Butstso ya kati eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wanadai kupuuzwa na viongozi wa kisiasa jambo ambalo wanawashauri wenzao kuwa macho kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wapya ifikapo mwaka wa 2022.
Wakiongea kwenye hafla ya mazishi ya Sheila Musundi wakiongozwa na Robert Amakobe na Nelson Amambia wenyeji hao wamekashifu kutokamilika kwa miradi za maendeleo na hivyo basi kushauri wakaazi eneo hilo kufanya mabadiliko ya uongozi kwa mnajili ya kuimarisha utendakazi wa eneo hilo
Aidha wanaelezea licha ya wao kuchagua viongozi kuwakilisha katika sekta mbalimbali wanazidi kupitia hali ngumu ya maisha ikiwemo kutokuwa na nyumba za kuishi jambo ambalo wameongezea kuwa ni kupitia tu uongozi bora wataweza kurejelea maisha yao kama watu wengine.
By Lindah Adhiambo