Chama cha kitaifa cha matabibu KUCO. chatishia kuandaa mgomo wa kitaifa alhamisi usiku wa manane.

Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa muda wa makataa uliopewa magavana kutia saini na kuanza kutekeleza utaratibu wa kurejea kazini uliotiwa saini kati ya matabibu na wizara ya afya wiki iliyopita.

Katibu mkuu wa chama cha taifa cha matabibu KUCO, Gorge Gibore akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi alitaja kuhangaishwa na baraza la magavana kuwa mojawapo wa sababu ya hao kugoma tena. Vilevile alitaja ukosefu wa nia njema na kujitolea kwa serikali za kaunti kusuluhisha zogo hilo na kurejesha hali ya kawaida katika sekta ya afya.

Kulingana na chama hicho cha matabibu, tarehe 5 mwezi huu wa Januari kiliipatia baraza la magavana muda wa saa 48 kuidhinisha utaratibu wa kurejea kazini kwa matabibu ulioafikiwa kati ya chama hicho na wizara ya afya, lakini baraza hilo likadinda kuandaa mkutano na matabibu hao.

Chama cha matabibu tarehe sita mwezi huu kiliitisha mkutano wa kusuluhisha mzozo uliopo kwa njia ya barua kwa baraza la magavana.

Mwenyekiti wa baraza la magavana Wycliffe Oparanya alitangaza kukataliwa mbali kwa makubaliano yaliokomesha mgomo wa matabibu ambao ulikwamisha huduma za afya humu nchini kwa siku 26.

Gibore alisema wana mipango ya kuandaa maandamano ya amani kote nchini kulalamikia kuto-tendewa haki matabibu na baraza la magavana

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE