LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Mwanaume kuwabaka bimti zake wawili

Katika kaunti ya Kirinyagah mwanaume ambaye aliwabaka bintize atajua hatima yake ijayo baada ya hakimu mkuu wa Baricho hakimu Anthony Mwicigi kuagiza ofisi ya urekebishaji tabia kuchunguza kisa hicho kwa kina.

Mmoja wa bintize  ana mtoto wa miezi saba na huyo mwingine ana ujaa uzito wa miezi sita.

Mshtakiwa John Gichira Gichini akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliomba msamaha kutoka kwa mahakama hiyo pamoja na familia yake kutokana na kitendo hicho, akilaumu shetani kwa kumpotosha.

“Ninasikitika sana kwa jinsi nimekosea familia yangu na ninaomba mahamaka hii inisamehe kwani kila binadamu anaweza kosea,” alisema Gichini.

Kesi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuamuliwa Alhamisi baada ya upande wa mashtaka kusema unahitaji kukabidhiwa vyeti vya kuzaliwa ili kubaini umri wa wasichana hao.

Kiongozi wa mashtaka aliwasilisha fomu ya P3, ripoti za ukaguzi wa kimatibabu na kadi za ubatizo kuunga mkono kesi hiyo.

Kesi hiyo itaamuliwa tarehe 14 mwezi huu.

Charles Oduor

Read Previous

KUCO kutishia kuandaa mgomo

Read Next

UMOJA WA ULAYA YAAGIZA DOZI MILLIONI TATU ZAIDI YA CHANJO ALMAARUFU BioNTechPfizer.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *