Waimbaji wa nyimbo za kidini kutoka eneobunge la Mumias Mashariki wanazidi kulalamikia hatua ya serikali ya kufunga makanisa na kusitisha ibaada Kama njia mojawapo ya kukabili msambao wa virusi vya corona
Wakiongozwa na Sammy Lumbasi waimbaji hao wameonyesha kutoridhika na namna serikali inavyo tekeleza amri hiyo
Kuhusu swala la masomo Lumbasi ametaka pawepo na uwazi kwenye shuguli za mashirika yanayowafadhili wanafunzi werevu wanaotoka jamii zisizo jiweza
Lumbasi vilevile ameitaka wizara ya elimu kutathmin upya na kumakinika swala la kuwateuwa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza mwezi ujao
By James Nadwa