Shughuli za kibiashara zilisitishwa kwa muda katika soko la shianda eneo bunge la Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega baada ya wafanyabiashara sokoni humo kuandamana wakilalamikia madai ya kuhangaishwa na maafisa wa polisi.

Wakiongozwa na Rose Papando na Peter Salasia wafanyabiashara hao wanadai kwamba maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi kuwafurusha kutoka sokoni humo kwa madai ya kuthibiti msambao wa virusi vya corona.

Wanasema inasikitisha kuona wakinyimwa nafasi ya kufanya biashara ili kutafuta pesa za kukimu mahitaji yao ya kila siku hasa wakati huu mgumu wa janga la virusi vya corona.

Kadhalika wamewashtumu maafisa wakuu wa polisi wanaohudumu eneo hilo kwa kufumbia macho masaibu wanayopitia.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE