Viongozi wa chama cha ANC katika kaunti ya Kakamega wameanzisha
Mikakati ya kusajili wanachama wapya wakilenga kukipa chama hicho
Nguvu mbele ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Wakiongea mjini Kakamega wakiongozwa na mkurugenzi wa ANC
Kaunti hii Isaac Otiende, wamesema lengo lao ni kuhakikisha kinara
Wa chama hicho Musalia Mudavadi anapata wafuasi wengi
Akijitayarisha kumenyana na viongozi wa vyama vingine kutwaa kiti
Cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kauli hiyo imeungwa mkono na kiongozi wa vijana eneo bunge la
Lurambi Joel Okwako na mwakilishi wa wanawake Ruth Ombayo.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya mwenyekiti wa ANC kaunti hii Titus
Khamala kudokeza kuwa zoezi hilo la usajili litazinduliwa rasmi
Mwezi Agosti mwaka huu.
By Imelda Lihavi