Wanakandarasi katika kaunti ya Bungoma wamemtaka mwanaharakati katika vuguvugu la Bungoma Liberation Zack Barasa kujitenga mbali na siasa katika kiwanda cha Machinjoni ya kuku katika eneo la Chwele.

Wakiongozwa na mwenekiti wao,Gabriel Wamalwa,wamesema kuwa eneo la Bungoma linahitaji waekezaji zaidi ili kuekeza katika eneo hili kusudi kuinua maisha ya wakaazi.akidai kaunti hii imesalia nyuma kimaendeleo kutokana na mvutano wa kisiasa .

Aidha ni usemi ambao umeungwa mkono na Anthony Masika mmoja wa wanakandarasi anayemtaka mwanaharakati huyo kugoma kuingiza siasa katika mradi huo,akidai muekezaji aliyekodesha kiwanda hicho cha kuku alipata kibali halali kutoka kwa serikali ya kaunti.

Yanajiri hayo,mwanaharakati Zack Barasa,akidaiwa kupinga kukodeshwa kwa kiwanda cha kuchinja kuku cha Chwele akidai serikali ya kaunti ya Bungoma haikufuata utaritibu mwafaka  wa sheria ya kukikodesha kiwanda hicho.

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE