Maafisa wa afisi ya bima ya afya NHIF  tawi la Bungoma  pamoja na wateja wao zaidi ya 40 wamepokea chanjo dhidi ya  virusi vya corona
kulingana na Collins Nyaranga mhudumu wa afya kutoka hospitali ya kibinafsi ya  Foundation  Healthcare  ambaye alikuwa akipeana chanjo hiyo ,idadi ya waliojitokeza kuipokea chanjo hiyo ni ya kuridhisha

 hivyo basi amewataka wakenya kukubali kupokea chanjo hiyo  haswaa wale walio na magonjwa ambatanishi kama vile kisukari na saratani  ili wajizuie na maambukizi mbali na kuisaidia serikali kudhibiti maambukizi hayo


waliopokea chanjo hiyo wameelezea sababu  za kukubali kupokea chanjo hiyo licha ya hofu inayosambazwa kuhusiana na chanjo hiyo

Hata hivyo  wamelezea kuwa na maswali mengi wanayohitaji  kung’amuliwa

By Hilary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE