Mamia ya wakulima wa miwa kutoka maeneo bunge ya Mumias Mashariki na Mumias Magharibi hii leo waliandamana kukashifu kile wanachodai ni njama kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa eneo hilo kuhujumu ufufuzi wa  kiwanda cha sukari cha Mumias.

Wakizungumza maeneo ya Shianda na Mumias mjini, wakulima hao wakiongozwa na Peter Salasia na Mohammed Osore wamesema kamwe hawatokubali juhudi za kufufua kiwanda hicho kudidimizwa kwani hatua hiyo huenda ikahujumu uchumi wa eneo hilo.

Haya yanajiri wakati ambapo mwekezaji kutoka kwa kampuni ya DEVKI steel company ambaye alikuwa amejitokeza kukifufua kiwanda hicho kwa kima cha shilingi bilioni 5 kujiondoa kwenye harakati za kuchukua usimamizi wa kiwanda hicho.

Mbunge wa Lugari Ayub Savula na mwenzake wa Lurambi Titus Khamala wamewataka wanasiasa kuondoa tofauti zao na kushirikiana kusaidia mwekezaji huyo kufufua kiwanda hicho.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE